🧡 Nenda kwenye maudhui makuu🔍 Nenda kwenye utafutaji

Tunafahamu umuhimu wa programu kutimiza mahitaji yako. Kwa kubuni kiolesura kinachopendeza na teknolojia changamano ya kisasa, tunajitahidi kuweka bidhaa za kuotomatisha kwenye Microsoft Windows ambazo ni rahisi kutumia na zinaweza kutimiza mahitaji.

Kikasha pepe cha Automation Workshop · v7.6.0

Automation Workshop

Kwa kuotomatisha majukumu yanayojirudia katika Windows, gharama hupunguzwa, na michakato huharakishwa kwa kuiunganisha kwenye mfumo mpya uliobuniwa unaoweza kusuluhisha mambo magumu bila watu kuhusika.

Hapa ndipo Automation Workshop inaingilia kati, kwa kuotomatisha hatua nyingi kwa njia maizi. Kuotomatisha majukumu hupunguza kuhusishwa kwa watu na pia muda unaopotezwa kwenye majukumu ya msingi. Kwa kuotomatisha majukumu, gharama hupunguzwa, na michakato hutekelezwa kwa haraka zaidi. Makosa ya watu na kuchelewa bila sababu huepukwa, na zana za kutazama hutolewa ili kukusanya maelezo kamili kuhusu michakato ya awali ya kiotomatiki.

Karakana, Vidhibiti vya Kumbukumbu na Foleni, Huduma na Majukumu…

Vipengele vya ajabu

Zana za ajabu

Kuanza

Kikasha pepe cha Command Line Email · v8.0

Command Line Email

Ukiwa na Command Line Email, unaweza kutuma jumbe za kawaida za maandishi na jumbe changamano za muundo wa HTML, kuambatisha faili, hati na picha kwenye barua pepe, kutuma barua pepe kutoka kwa Majukumu Yaliyoratibiwa, hati za CGI au programu yoyote inayoweza kutekeleza amri za nje.

Vipengele mahiri vinaruhusu utumiaji wa vigezo kutoka kwenye faili ya maandishi, kusimba maandishi ya ujumbe (Unicode, UTF-8, nk.), kutumia usimbaji wa MIME (Multipurpose Internet Mail Extensions), kutumia mbinu kadhaa za uthibitishaji, kama vile AUTH PLAIN, LOGIN, NTLM, CRAM-MD5, na kutambua kiotomatiki, na kuweka kipindi salama cha mawasiliano na seva ya SMTP kwa kutumia vipengele salama vya SSL au STARTTLS, ikiwemo idadi bila kikomo ya wapokeaji wa TO, CC na BCC.

Kwa muhtasari

  • Tuma barua pepe zenye vipengele kamili na viambatisho bila kikomo, muundo wa HTML na uthibitishaji wa barua pepe kutoka kidokezo cha DOS.
  • Weka kigezo chochote cha barua pepe ukitumia faili za nje za maandishi, zenye uwezo kamili wa kutumia Unicode na UTF-8.
  • Uthibitishaji wa SMTP wenye kipengele cha kutambua kiotomatiki ili kubaini muunganisho na seva ya SMTP kiotomatiki au kutumia mbinu za uthibitishaji za LOGIN, PLAIN, NTLM, na CRAM-MD5.
  • Muunganisho salama ukitumia STARTTLS na SSL usimbaji wa data wenye utatuzi mahiri.
  • Vigezo rahisi vya mfumo wa amri vinavyoruhusu majina.
  • Tumia faili za makundi kutuma barua pepe kutoka programu* yoyote, zikiwemo VBA, PHP, hati za Perl na zaidi…

Kuanza

Kuhusu

Febooti, Ltd. ni kampuni ya kibinafsi, inayopatikana Ulaya. Lengo letu kila mara huwa ubora wa bidhaa. Kuanzia hatua ya kuzingatia kwa makini utendaji na kiolesura hadi kufanyia majaribio matokeo, kila hatua huchukuliwa kwa uadilifu ili kutoa huduma ya kuotomatisha yenye uhakika.

Wasiliana nasi

Tunathamini maoni yako na tunakuomba uwasiliane nasi iwapo una maoni, mapendekezo na maswali.