Video · Angalia jinsi ilivyo rahisi kufuatilia seva ya FTP ili kuona faili mpya. Pindi faili mpya itakapoonekana katika saraka ya seva ya FTP, hupakuliwa na kuambatishwa kwenye ujumbe wa barua pepe.
Haya yote hufanyika kiotomatiki—hamna ujuzi wa kuandika msimbo ya programu. Elekeza tu na ubofye ili kuanzisha Jukumu lako la kwanza la kiotomatiki!
Kiolesura maizi chenye zana za kubuni Majukumu na Vielelezo vya mipangilio kitakuelekeza katika mchakato wa kusanifu Jukumu bila kuhitaji ujuzi wa kuandika hati au mafunzo ya utangulizi. Ni rahisi kuotomatisha kitu chochote na mahali popote ukitumia mfumo huu wa kuotomatisha usiohitaji misimbo.
Utangulizi
- Umechoshwa na kazi za kujirudia?
- Tuseme ungependa kuotomatisha uchakataji wa ankara zinazofikia seva yako ya FTP.
- Febooti Automation Workshop inazishughulikia.
Tazama seva ya FTP
- kisha uchague FTP Watcher (Kitazama FTP) kwenye orodha ya Vichochezi.
- Weka eneo la folda, maudhui unayotaka kufuatilia, na maski ya faili.
- Kisha, weka anwani ya seva yako, pamoja na jina la mtumiaji na nenosiri.
- Kichochezi kiko tayari!
Otomatisha upakuaji
- Hebu sasa tuongeze Vitendo itakavyotekeleza.
- Automation Workshop inaruhusu zaidi ya Vitendo 100 tofauti lakini tunachotaka ni Download File (Pakua Faili).
- Bofya sehemu ya Remote File (Faili ya Mbali), tumia Variable Wizard, chagua Kitazama FTP kwenye orodha ya Vichochezi kisha uchague folda ambako faili inaweza kuhifadhiwa.
Otomatisha barua pepe
- Unachohitaji kufanya sasa ni kuweka mipangilio yake ili ankara itumwe kiotomatiki kwenye idara yako ya Uhasibu.
- Chagua Send Mail (Tuma Ujumbe) kwenye orodha ya Vitendo, andika kiolezo cha ujumbe na kisha uchague sehemu ya Kiambatisho.
- Tumia tu Variable Wizard kisha chagua Pakua Faili katika sehemu ya Action (Vitendo).
Muhtasari
- Kisha lipe Jukumu jina na ukamilishe kuandaa.
- Tayari! Inafanya kazi!
- Sasa, baada ya ankara mpya kupakiwa kwenye folda, itatumwa kwenye idara yako ya Uhasibu kiotomatiki!
Inapatikana kote duniani
Kiratibu cha kina cha kazi—Automation Workshop hufanya kazi vyema katika matoleo yote ya kisasa ya biti 32 na 64 ya Microsoft Windows: Windows 10 · Windows 11 · Server 2016 · Server 2019 · Server 2022.
Matoleo ya zamani ya Windows (kama vile Windows 8 na Server 2008) hayatumiki "rasmi" lakini bado yanapaswa kufanya kazi vizuri. Usanifu wa Windows unabadilika na programu zetu zimebuniwa kufanya kazi na matoleo ya zamani na ya kisasa.